Saturday, October 22, 2011

FAIDA ZA KILIMO.

Kilimo ni shighuli ya  mwanzo ya binaadamu.Kilimo kina umuhimu mkubwa sana kwa binaadamu kutokana na faida    zifuatazo:  
  1. Humpatia binaadamu chakula.Binaadamu hawezi kufanya shughuli yoyote kama hana  chakula cha kuweza kula iliapate nguvu zakuzalisha.Na chakula hiki hakiwezi kupatikana sehemu yoyote zaidi ya shambani.
  2. Humpatia binaadamu mali ghafi.Kwa mfano zao kama pamba linatumika kama malighafi ya kutengenezea nguo mbalimbali
  3. Humpatia binaadamu kipato kwa kuuza mazao ambayo ameyalima kutoka shambani kwake kwa kuuza katika masoko mbalimbali ndani na nje ya nchi.
  4. Huipatia serikali fedha za kigeni kwakuuza mazao mbalimbali katika soko la dunia.
Hizo ni baadhi tu ya faida za kilimo  ingawa ziko nyingi sana.

NB: KILIMO NI UTI WA MGONGO WA TAIFA LOLOTE DUNIANI HIVYO NINGEPENDA KUWASHAURI WATANZANIA KUWEKEZA KATIKA KILIMO KWANI WASHWAHILI WANASEMA "JEMBE HALIMTUPI MTU"



PICHA ZA KILIMO TANZANIA   
MAZAO YA MATUNDA MBALIMBALI

ZAO LA NDIZO

ZAO LA KAHAWA

ZAO LA VIAZI NA KAROTI

ZAO LA MAHINDI

ZAO LA NYANYA


Wednesday, October 19, 2011

SAMAKI SAMAKI SAMAKI

Samaki ni kiumbe cha zamani sana.Na inasadikiwa kuwa samaki alianza kuishi miaka milioni 500 iliyopita. Hivi ni viumbe vya majini.  Samaki kupumua kwa kutumia gills.Samaki hutumia mimea ya baharini   kulisha samaki wadogo, wakati baadhi ya samaki kama  shark hutegemea juu ya samaki wengine.Kuna aina kubwa ya samaki, tofauti katika sura ya kawaida, na rangi.Samaki wana ukubwa mbalimbali kutoka 8 mm hadi mita 16.
Samaki wamegawanyika katika  makundi mengi,kati ya hayo ni:


  • SAMAKI WA MAJI BARIDI
Hawa ni samaki wanaopatikana katika mito,maziwa amabapo kuna kuwa na hali ya uchumvi 0.05%.Na aslilimia 41 ya samaki wanaishi katika maji baridi.



  • SAMAKI WA BAHARINI
Hawa ni samaki wanaoishi baharini.Kuna aina nyingi za samaki wa baharini karibia 15,000.Samaki hawa hutofautiana kutokana na muonekano wao wa rangi pamoja na miundo ya miili yao.

Sunday, October 16, 2011

Maisha ni mambo yafuatayo

Ndugu zangu karibuni katika siku nyingine tena katika Amah Blog ambapo tutaelezana mambo mbalimbali yanayohusu maisha ya vijana na maendeleo yao kwa ujumla.Bila ya kusahau tukumbuke sisi vijana ni sehemu muhimu sana katika jamii yoyote.Mafanikio ya vijana ndio maendeleo ya taifa lolote duniani.Hivyo basi hatuna budi kuhamasishana katika mambo mazuri kwa manufaa ya taifa letu.Ama leo ningependa kueleza mambo ambayo yanaweza kumlketea kijana maendeleo.
  • Kufanya kazi kwa bidii


Hili ni jambo la kwanza kabisa kijana anatakiwa alizingatie katika maendeleo yake.Ili upate maendeleo hakikisha unawajibika ipasavyo wewe kijana katika sekta yoyote ile uliyokuwa nayo.Kama ni mwalimu fundisha kwa juhudi.Kama ni mwanafunzi soma kwa bidii.Kama ni mfanyakazi wa sekta yoyote fanya kazi kwa nguvu zote bila ya uvivu ,majivuno,utoro na mabo yote yanayorudisha nyuma maendeleo.
  • Kuacha tamaa na mabo yote ya kuiga
Sasa hivi kuna mambo mengi yanatokea katika ulimwengu amabyo sio mazuri katika jamii.Wewe kama kijana unatakiwa uache kuyaiga mambo hayo amabye sio mazuri na ukumbuke ya kuwa tamaa na mbo ya kuiga yanaweza kukupelekea kupata hasara na majuto makubwa katika maisha yako kama vile magonjwa hatari hatimae kifo.
  • Kuwa na msimamo na malengo
Vilevile unatakiwa uwe na malengo pamoja na plani kwani nothing is impossible under the sun cha msingi nim kuwa na msimamo juu ya yale malengo yako uliyoyapanga
  • Adabu na utii
Hii ni nyenzo muhimu sana katika mafanikio ya mtu wowote hasa hasa huu wakati tulionao.Kijana unatakiwa umuheshimu mtu yeyote bila ya kujali  pesa wala cheo cha huyo mtu unaemuheshimu.Na usimzarau kwa ufukara wake mtu yeyote kwani hujuim kesho atakuwa nani
  • Kumtii Mungu muumba
Hili ni jambo muhimu sana kwani jitihada zetu zote za duniani hazitakuwa na mafanikio kama zitakuwa na mafanikio basi hazitakuwa na baraka ikiwa sisi tunamdharau yule aliyetuleta hapa duniani. 
Kwa leo ningependa tuishie hapa wadau.


Tourism In Tanga Region.

Tanga is among the Tanzania region in which there are many tourist attraction.When you travel in Tanga you will see many tourist attractions like caves,rivers and many beaches.
Below are the some of tourist attraction found in Tanga.

Amboni Cave
 
Above are the pictures of Amboni looks from the outside view.This cave is found at Tanga district in Tanga region.

Jet beach

This is a picture of bridge used by the Mbolea company found in Tanga to import materials for manufacturing fertilizer.Now a day this bridge has been broken so is not used.At left side of this bridge there is a beach known as Jet beach.This beach is used by both citizens and foreign to rest at the days of Saturday and Sunday due to hard working on the working days.Also this beach is among tourist attraction since it is very beautiful beach in Tanga.

Sadani

Thursday, October 13, 2011

This is very good blog I didn't see before