Ndugu zangu karibuni katika siku nyingine tena katika Amah Blog ambapo tutaelezana mambo mbalimbali yanayohusu maisha ya vijana na maendeleo yao kwa ujumla.Bila ya kusahau tukumbuke sisi vijana ni sehemu muhimu sana katika jamii yoyote.Mafanikio ya vijana ndio maendeleo ya taifa lolote duniani.Hivyo basi hatuna budi kuhamasishana katika mambo mazuri kwa manufaa ya taifa letu.Ama leo ningependa kueleza mambo ambayo yanaweza kumlketea kijana maendeleo.
- Kufanya kazi kwa bidii
Hili ni jambo la kwanza kabisa kijana anatakiwa alizingatie katika maendeleo yake.Ili upate maendeleo hakikisha unawajibika ipasavyo wewe kijana katika sekta yoyote ile uliyokuwa nayo.Kama ni mwalimu fundisha kwa juhudi.Kama ni mwanafunzi soma kwa bidii.Kama ni mfanyakazi wa sekta yoyote fanya kazi kwa nguvu zote bila ya uvivu ,majivuno,utoro na mabo yote yanayorudisha nyuma maendeleo.
- Kuacha tamaa na mabo yote ya kuiga
Sasa hivi kuna mambo mengi yanatokea katika ulimwengu amabyo sio mazuri katika jamii.Wewe kama kijana unatakiwa uache kuyaiga mambo hayo amabye sio mazuri na ukumbuke ya kuwa tamaa na mbo ya kuiga yanaweza kukupelekea kupata hasara na majuto makubwa katika maisha yako kama vile magonjwa hatari hatimae kifo.
- Kuwa na msimamo na malengo
Vilevile unatakiwa uwe na malengo pamoja na plani kwani nothing is impossible under the sun cha msingi nim kuwa na msimamo juu ya yale malengo yako uliyoyapanga
- Adabu na utii
Hii ni nyenzo muhimu sana katika mafanikio ya mtu wowote hasa hasa huu wakati tulionao.Kijana unatakiwa umuheshimu mtu yeyote bila ya kujali pesa wala cheo cha huyo mtu unaemuheshimu.Na usimzarau kwa ufukara wake mtu yeyote kwani hujuim kesho atakuwa nani
- Kumtii Mungu muumba
Hili ni jambo muhimu sana kwani jitihada zetu zote za duniani hazitakuwa na mafanikio kama zitakuwa na mafanikio basi hazitakuwa na baraka ikiwa sisi tunamdharau yule aliyetuleta hapa duniani.
Kwa leo ningependa tuishie hapa wadau.
No comments:
Post a Comment